FUNUNU DANGOTE KUINUNUA ARSENAL




Bilionea Namba moja Afrika raia wa Nigeria, Aliko Dangote ndoto yake ya kumiliki club ya soka ya Arsenal ya England bado haijafutika na leo August 17, 2017 ameripotiwa na mtandao wa express.co.uk amesema kama akifanikiwa kuinunua Klabu hiyo atamfuta kazi kocha Arsene Wenger.

Arsene Wenger
Dangote mwenye umri wa miaka 60 ameweka wazi mpango wake huo kwa Arsene Wenger kutokana na kutoona mafanikio yoyote ya kocha huyo>>>“Kitu cha kwanza nitakachobadili Arsenal ni kocha, ni kweli Wenger amefanya kazi nzuri lakini lazima aje kocha mwingine ajaribu bahati yake.”

Aliko Dangote
Bilionea Dangote kwa sasa ili lengo lake lifanikiwe anahitaji kuwashawishi Stan Kroenke anayemiliki asilimia 65 ya hisa za Arsenal na Alisher Usmanov anayemiliki asilimia 30 ya hisa kuiuza club hiyo. Kama utakumbuka vizuri Arsene Wenger ambaye amekuwa hafanyi vizuri kwa sasa amedumu na Arsenal tangu 1996.
FUNUNU DANGOTE KUINUNUA ARSENAL FUNUNU DANGOTE KUINUNUA ARSENAL Reviewed by MIKASA_SIMULIZI on August 17, 2017 Rating: 5

No comments

Search Blog